Waziri Mkuu mpya wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, Rami Hamdallah
amelaani mpango wa utawala haramu wa Israel wa kutaka kujenga vitongoji
vipya katika ardhi za Wapalistina unazozikalia kwa mabavu. Rami amesema
hatua kama hiyo itaendelea kudidimiza matumaini ya kuwa na madola mawili
kama njia ya kutatua kadhia ya Palestina. Makundi ya kijamii ya
Palestina yamesema yataandamana kupinga vikali hatua hiyo.
Hii ni katika
hali ambayo, baraza la walowezi wa Kizayuni limemtaka Waziri Mkuu wa
utawala ghasibu wa Israel, Benjamin Netanyahu aidhinishe ujenzi wa
nyumba 550 katika eneo la Bruchin. Kuendelea ujenzi wa vitongoji vya
Wazayuni katika ardhi za Wapalestina kumelaaniwa na Umoja wa Mataifa
pamoja na taasisi zingine muhimu za kimataifa lakini utawala huo haramu
umeendelea kutia pamba masikioni kutokana na uungaji mkono unaopata
kutoka kwa Marekani na waitifaki wake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment