Serikali ya Sudan imekubali pendekezo la Umoja wa Afrika kwa ajili ya
kutatua tofauti zake na Sudan Kusini. Sudan imewasilisha rasmi suala
hilo kwa Thabo Mbeki Rais wa zamani wa Afrika Kusini ambaye ni
mpatanishi wa AU katika mazungumzo ya amani ya nchi mbili hizo na
kumjulisha utayarifu wake wenye lengo la kutatua tofauti zilizopi kati
ya pande mbili. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan
AbubakarEl-Saddiq Muhammad Amin amesema, Thabo Mbeki amesisitiza ulazima
wa kuainishwa eneo la mpakani lisilokuwa la kijeshi kwa kipindi cha
miezi sita kati ya nchi mbili hizo.
Aidha AU imepenekeza pia kuchunguza
kadhia ya uungaji mkono wa Juba kwa makundi ya waasi ambapo Khartoum na
Juba zimetakiwa kuwasilisha mapendekezo yao kwa umoja huo. Umoja wa
Afrika pia, umezitaka nchi mbili, kusitisha uungaji mkono wowote kwa
makundi ya waasi, ili kutoa fursa ya kutekelezwa makubaliano ya amani
yaliyotiwa saini na viongozi wa nchi mbili mwaka jana huko mjini Addis
Ababa, Ethiopia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment