Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani Henry Kissinger
amesema kuwa vyombo vya habari vya nchi hiyo vinasema urongo kuhusu hali
ya mambo nchini Syria.
Kissinger ambaye alikuwa akihutubia katika Chuo Kikuu cha Michigan
amesema, vyombo vya habari vya Marekani vinapotosha ukweli wa mambo na
havisemi ukweli kuhusu habari zinazohusiana na Syria.
Amesema kuwa vyombo hivyo vinamtambulisha Rais Bashar Assad wa Syria
kuwa ni dikteta anayeua wananchi wake na kwamba waasi ni wanademokrasia.
Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani amesema upotoshaji huo
unafanyika katika fremu ya siasa makhsusi.
Matamshi hayo ya Kissinger yametolewa wakati Marekani inakosolewa kwa
kuchochea fitina za kimadhehebu nchini Syria na katika nchi nyingine za
Mashariki ya Kati kwa kuingilia mambo ya ndani ya nchi hizo.
No comments:
Post a Comment