Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa nchi za Afrika zimeshuhudia ongezeko la uwekezaji wa kigeni katika mwaka uliopita wa 2012.
Umoja wa Mataifa umesema uwekezaji wa kigeni katika nchi za Afrika
uliongezeka kwa dola bilioni 50 katika mwaka 2012. Taarifa ya UN imesema
kuwa, nchi za Afrika ni miongoni mwa nchi ambazo zina ustawi mkubwa
zaidi wa uchumi duniani.
Ripoti hiyo inasema kuwa ustawi wa uchumi wa nchi za Afrika
umepatikana katika hali ambayo uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni
katika nchi mbalimbali za dunia katika mwaka 2012 umepungua kwa asilimia
18.
Aprili mwaka huu pia Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) ulitangaza kuwa uchumi wa nchi za Kiafrika unaendelea kustawi vizuri.
No comments:
Post a Comment