Kambi ya upinzani nchini Guinea Conakry imetangaza kuwa
haitafanya mazungumzo ya aina yoyote ya wawakilishi wa serikali ya nchi
hiyo ila baada ya kudhaminiwa usalama wa viongozi wake.
Viongozi wa kambi ya upinzani nchini Guinea wamesema kuwa sharti la
kufanya mazungumzo na serikali ya Conakry ni kudhaminiwa usalama kamili
wa viongozi wa upinzani.
Msemaji wa muungano wa kambi ya upinzani Abu Bakr Silla amesema
viongozi wa kambi hiyo wameamua kusitisha mazungumzo ya kitaifa hadi
pale watakapopewa madhamana ya usalama wao na kuondolewa vizingiti vyote
vinavyowakabili.
Amekosoa ukandamizaji unaofanywa na serikali dhidi ya wanaharakati wa
vyama vya upinzani na kusisitiza kuwa ni ukiukaji wa sheria za nchi.
No comments:
Post a Comment