Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas imetangaza kuwa,
viongozi wa harakati ya Fat-h huko Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan,
Misri na Ukanda wa Gaza wanafanya njama za kuichafua sura ya Hamas,
ndani na nje ya Palestina na hasa nchini Misri. Sami Abu Zuhri Msemaji
wa Hamas amekanusha madai yanayotolewa na Fat-h kwamba Hamas inajiingiza
katika masuala ya ndani ya Misri.
Abu Zuhri ameongeza kuwa, vibaraka wa
utawala uliopinduliwa wa Hosni Mubarak na viongozi wa Fat-h
wanashirikiana katika kutekeleza njama hizo, ili Hamas ionekane kuwa ni
adui mbele ya wananchi wa Misri. Amesisitiza kuwa siasa za nje za Hamas
ni kutoingilia masuala ya ndani ya nchi yoyote ile ya Kiislamu na
Kiarabu. Aidha Msemaji wa Hamas amevitaka vyombo vya sheria vya Misri
kuwasaka na kuwatia mbaroni watu wote waliohusika katika kuwatesa
Wapalestina walioko nchini Misri.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment