Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Abbas Araqchi, amepuuzilia
mbali matamshi ya hivi karibuni ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada,
John Baird, kuhusu uchaguzi wa rais uliofanyika Juni 14 katika Jamhuri
ya Kiislamu. Katika matamshi yake hivi karibuni, Baird ambaye ana tabia
ya kutoa matamshi ya kijeuri ya kuuingilia mambo yasiyomuhusu, alidai
kuwa, uchaguzi wa Rais Iran eti haukuwa na maana.
Msemaji wa Wizara
Mambo ya Nje ya Iran alipoulizwa kuhusu matamshi hayo ya Waziri wa Mambo
ya Nje wa Canada amesema, haoni haja hata ya kujibu matamshi hayo.
Amesema waziri huyo wa Canada ana tabia ya kutoa matamshi kama hayo
jambo ambalo linatilia shaka uwezo wake wa kutathmini masuala ya
kisiasa. Kuhusu machafuko yanayoendelea hivi sasa nchini Uturuki,
Araqchi ametoa mwito kwa wananchi wa Uturuki na serikali ya nchi hiyo
kujizuia kueneza mgogoro uliopo. Amekanusha madai kuwa Iran inaingilia
masuala ya ndani ya Uturuki na kusema, Waziri Mkuu wa Uturuki Recep
Tayyip Erdogan anapaswa kutii matakwa ya wananchi. Akijibu swali kuhusu
iwapo sera za kigeni za Iran zitabadilika baada ya kuchaguliwa Sheikh
Hassan Rohani kama rais, Araqchi amesema, sera za kigeni za Jamhuri ya
Kiislamu zina msingi unaotegemea thamani na maslahi ya kitaifa na
miongozo ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, na hivyo mkondo
utaendelea kuwa huo isipokuwa mbinu za utekelezaji ndizo zinazoweza
kubadilika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment