China imesema kuwa, itafanya kila linalowezekana ili kuzisaidia
Sudan na Sudan Kusini kufikia mapatano na hivyo kumaliza suutafahumu na
hitilafu kati ya pande mbili hizo.
China imesema hayo leo kufuatia hatua ya hivi karibuni ya Sudan ya
kukataa kusafirisha mafuta ya Sudan Kusini kupitia mabomba yake.
Ali Karti, Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan juzi alimueleza Zhong
Jianhua, Mjumbe wa China barani Afrika kwamba, Sudan imeanzisha jitihada
zote ili kufikia uhusiano wema na jirani yake Sudan Kusini.
Mjumbe wa China barani Afrika amesema kuwa, nchi yake itafanya kila
linalowezekana ili kuziwezesha Khartoum na Juba kufikia mapatano na
kutatua masuala yaliyosalia baina yao.
No comments:
Post a Comment