Msemaji wa Rais Hamid Karzai wa Afghanistan amesema kuwa, nchi
hiyo imesimamisha mazungumzo na Marekani kuhusiana na makubaliano ya
pande mbili ya kiusalama (BSA) kutokana na misimamo ya Washington. Amal
Faizi amesema kuwa, kuna tofauti kati ya kile kinachosemwa na serikali
ya Marekani na hatua inazochukua kuhusiana na mazungumzo ya amani ya
Afghanistan.
Hayo yamejiri baada ya kuripotiwa mazungumzo ya moja kwa moja kati ya
maafisa wa Marekani na wanamgambo wa kundi la Taliban. Pia Rais wa
Afghanistan amekosoa kitendo cha kupewa Taliban ofisi ya kisiasa katika
mji mkuu wa Qatar, Doha. Suala hilo pia limepingwa na wabunge wa
Afghanistan. Karzai amesema serikali yake haitoshiriki mazungumzo yoyote
na Marekani pamoja na kundi la Taliban hadi pale mazungumzo hayo
yatakapoongozwa na serikali ya Kabul.
No comments:
Post a Comment