Rais Barack Obama wa Marekani ametoa wito wa kufanywa jitihada za kupunguza silaha za nyuklia za nchi yake pamoja na Russia.
Akizungumza huko Brandenburg Gate katika safari yake kwenye mji mkuu
wa Ujerumani, Berlin, Obama amesema kuwa ana uhakika Marekani inaweza
kulinda usalama wake hata kama itapunguza silaha zake za nyuklia hadi
theluthi moja na kuitaka Russia pia kufanya hivyo hivyo.
Matamshi hayo ya Obama yamejibiwa haraka na Naibu Waziri Mkuu wa
Russia Dmitry Rogozin aliyesema kwamba, wito huo wa Obama wa kupunguza
silaha za nyuklia hauwezi kuzingatiwa. Ameongeza kuwa, hatua ya Marekani
ya kupelekea mitambo ya kuzuia makombora barani Ulaya ni kikwazo
kikubwa cha kupunguza silaha za nyuklia kwa Russia.
Kremlin imesema kwamba, suala la kupunguzwa hifadhi kubwa ya silaha
za nyuklia, halipaswi kuishia tu kwa nchi hizo mbili, bali linapaswa
kujumuisha serikali nyingine zinazohodhi silaha hizo hatari.
No comments:
Post a Comment