Waziri Mkuu wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, Salam Fayyad amejiuzulu
baada ya kuhudumu kwenye wadhifa huo tangu 2007. Habari zinasema kuwa,
Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, Mahmoud Abbas amekubali barua ya
kujiuzulu Waziri Mkuu huyo ingawa amemtaka kubakia katika nafasi hiyo
hadi pale Waziri Mkuu mpya atakapoteuliwa. Uhusiano wa Fayyad na Abbas
umekuwa wa mkwaruzano katika siku za hivi karibuni. Mwezi uliopita,
Fayyad alikubali barua ya kujiuzulu Waziri wa Fedha, Nabil Qassis lakini
Abbas akakataa kuipokea barua hiyo.
Hata hivyo hatua ya Waziri Mkuu
huyo ya kujiuzulu si jambo geni kwani mara kadhaa amekuwa akiandika
barua ya kujiuzulu lakini kutokana na mashinikizo ya Marekani amekuwa
akilazimika kubakia ofisini.
No comments:
Post a Comment