Siku kama ya leo miaka 85 iliyopita, sawa na tarehe 24 Aprili 1927 iligunduliwa chanjo ya BCG. Chanjo hiyo iligunduliwa na Calmette na Guerin madaktari bingwa wa Ufaransa, baada ya kufanya utafiti kwa miaka kadhaa. Sio vibaya kukumbusha hapa kuwa, chanjo ya BCG inatumika kwa ajili ya kuzuia maradhi ya kuambukiza ya kifua kikuu, na baada ya kugunduliwa chanjo hiyo kasi ya maambukizi ya maradhi hayo pamoja na idadi ya watu waliokuwa wakifariki dunia kutokana na kifua kikuu ikapungua duniani kote.
Siku kama ya leo miaka 1240 iliyopita alifariki dunia Haroun Rashid mmoja wa makhalifa wa utawala wa Kiabbasi. Harun Rashid alishika hatamu za uongozi mwaka 170 Hijiria na mwanzoni mwa utawala wake alikuwa chini ya ushawishi wa mama yake. Baada ya kufa mama yake llimteua Yahya Barmaki kuwa msimamizi wake na kuanzia hapo masuala yote ya ukhalifa yakawekwa mikononi mwa Yahya na wanawe. Haroun Rashid alikuwa mpenda anasa na wakati huo huo mwenye nguvu na aliamiliana kidhalimu na kikatili na Ahlul Bait wa Mtume Mtukufu (saw) na wafuasi wao, kwa kadiri kwamba aliua shahidi idadi kubwa ya watu hao katika jela zake za kuogofya. Hatimaye Haroun Rashid aliangamizwa wakati akielekea Khorasan mashariki mwa Iran kwa ajili ya kuzima uasi wa wapinzani wake.
Na miaka 741 iliyopita katika siku kama ya leo, inayosadifiana na tarehe 24 Aprili mwaka 1271, mtalii Marco Polo wa Venice alianza safari ya kihistoria ya kutembelea bara la Asia. Kabla yake baba na ami yake walitembelea China kupitia njia ya Asia Ndogo na Iran. Baada ya kurejea ndugu wa Polo kutoka Ulaya, Marco Polo akifuatana na baba yake kwa mara nyingine walielekea China na kutembelea nchi hiyo na visiwa vya kusini mashariki mwa Asia. Baada ya kurejea nchini kwake, Marco Polo aliandika kumbukumbu ya safari iliyoitwa "Maajabu" kuhusiana na hali ya kijiografia ya ardhi za China, Turkmenistan, Mongolia na sehemu za kusini mashariki mwa Asia. Safari ya Marco Polo barani Asia ilichukua karibu miaka 20. Siku kama ya leo miaka 1240 iliyopita alifariki dunia Haroun Rashid mmoja wa makhalifa wa utawala wa Kiabbasi. Harun Rashid alishika hatamu za uongozi mwaka 170 Hijiria na mwanzoni mwa utawala wake alikuwa chini ya ushawishi wa mama yake. Baada ya kufa mama yake llimteua Yahya Barmaki kuwa msimamizi wake na kuanzia hapo masuala yote ya ukhalifa yakawekwa mikononi mwa Yahya na wanawe. Haroun Rashid alikuwa mpenda anasa na wakati huo huo mwenye nguvu na aliamiliana kidhalimu na kikatili na Ahlul Bait wa Mtume Mtukufu (saw) na wafuasi wao, kwa kadiri kwamba aliua shahidi idadi kubwa ya watu hao katika jela zake za kuogofya. Hatimaye Haroun Rashid aliangamizwa wakati akielekea Khorasan mashariki mwa Iran kwa ajili ya kuzima uasi wa wapinzani wake.
No comments:
Post a Comment