Licha ya maandamano makubwa ya wananchi wa Ufaransa ya kupinga
kuhalalishwa kisheria ndoa za watu wanaolawitiana, bunge la taifa la
nchi hiyo limepasisha mswada wa sheria hiyo kwa wingi mkubwa wa kura.
Bunge la Ufaransa limepasisha kwa kura 249 za 'ndiyo' dhidi ya 97 za
'hapana' mswada wa sheria inayowaruhusu kuoana kisheria wanaume
wanaolawitiana. Kama ilivyokuwa imetarajiwa, wabunge wa chama cha
kisoshalisti, chama cha kijani na cha mrengo wa kushoto waliunga mkono
mswada huo uliopingwa na wawakilishi wa chama cha umoja kwa ajili ya
harakati ya wananchi. Wabunge wa mrengo wa kulia wameeleza wasiwasi
walionao kutokana na kupasishwa mswada huo. Kupasisha sheria ya kuruhusu
ndoa za watu wanaolawitiana ni moja ya ahadi zilizotolewa na Rais
Francois Hollande wa Ufaransa wakati wa kampeni za uchaguzi kwa
madhumuni ya kuvutia kura za makundi ya watu wa jinsia moja wenye
mwenendo potofu wa maingiliano ya kimwili…/
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment