Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Sunday, February 3, 2013

Obama aonekana akitumia bunduki

Hatua ya Rais Barack Obama wa Marekani kuonekana akifanya mazoezi ya kulenga shabaha kwa bunduki, imetajwa zaidi na weledi wa masuala ya kisiasa kuwa ni inayounga mkono vitendo vya matumizi ya silaha nchini humo.
Picha hizo zilisambazwa na Ikulu ya White House na kuwatia wasi wasi mkubwa wanaharakati wanaoitaka serikali ya Washington kupitisha muswada wa sheria utakaopiga marufuku matumizi ya silaha kwa raia. Kufuatia mauaji hivi karibuni katika shule ya msingi katika wilaya ya New Town katika jimbo la Connecticut, Rais Barack Obama wa Marekani aliahidi kuchukua hatua madhubuti kwa ajili ya kupunguza vitendo vya kikatili vinavyotokana na matumizi ya silaha za moto. Hata hivyo kauli hiyo ilikabiliwa na radiamali hasi kutoka kwa lobi ya waungaji mkono wa matumizi hayo ya bunduki nchini humo. Weledi wanaamini kuwa, hatua ya rais huyo kuonekana akifanya mazoezi ya kulenga shabaha kwa bunduki inakinzana na kauli yake ya kupunguza vitendo vya kikatili nchini Marekani.

No comments: