Rais wa Ufaransa Francois Hollande ambaye vikosi vya nchi yake vimevamia
Mali kwa kisingizio cha kupambana na waasi, amesema kuwa, vita vya
Ufaransa nchini humo havijamalizika. Rais Hollande aliyasema hayo jana
katika medani ya Uhuru mjini Bamako, mji mkuu wa Mali. Ameongeza kuwa,
kadhia ya kushambulia Mali ilifikiwa mnamo tarehe 10 mwezi jana na
kwamba, askari wa nchi yake wataendelea kubakia Mali kupambana na waasi.
Hollande amedai kuwa, Ufaransa imeishambulia Mali kwa ushirikiano na
jamii ya kimataifa chini ya uungaji mkono wa nchi za Ulaya.
Akiwa mjini
Timbuktu kaskazini mwa Mali, rais huyo wa Ufaransa alisema kuwa, vikosi
vya nchi hiyo vitaendelea na operesheni zake Mali na kwamba vitakabidhi
kwa awamu hatamu za uendeshaji operesheni hizo vikosi vya askari
wapatao 8,000 wa nchi za Afrika. Nchi zinazounga mkono vita vya Ufaransa
nchini Mali ni pamoja na Marekani, Canada, Uingereza, Ubelgiji,
Ujerumani na Denmark. Weledi wa mambo wanasema lengo la vita vya Mali ni
kupora utajiri mkubwa wa mali asili nchini humo kama vile mafuta,
dhahabu na madini ya urani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment