Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah nchini
Lebanon amesema kuwa, imepangwa mikakati maalumu ya kumvunjia heshima
Mtume Mtukufu Muhammad SAW na dini tukufu ya Kiislamu na jambo hilo
linatoa changamoto kubwa kwa umma wa Kiislamu. Akihutubia kwa mnasaba wa
kuanza Wiki ya Umoja wa Kiislamu na kuzaliwa Mtume Mtukufu SAW huko
kusini mwa Lebanon, Sayyid Hassan Nasrullah amesisitiza kuwa Qurani
Tukufu inatulingania kufanya mazungumzo baina yetu, amma suala la
kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu, kamwe halikubaliki kwa mtu
yeyote yule.
Sayyid Nasrullah ameongeza kuwa changamoto nyingine
inayoukabili ulimwengu wa Kiislamu ni ongezeko la mapigano na machafuko
kwenye nchi za ulimwengu wa Kiislamu na Kiarabu. Katibu Mkuu wa
Hizbullah amesema kuwa, machafuko na mapigano mengi yanajiri kwa
malengo ya kisiasa, ingawa yanafanyika kwa kisingizio cha umadhehebu na
udini. Ameongeza kuwa,mapigano hayo yanafanyika kwa lengo la kujipatia
madaraka na wala hakuna mahusiano yoyote na Uislamu, Ukristo na wala
usuni na ushia. Nasrullah ameongeza kuwa, mapigano yanayotokea katika
nchi mbalimbali kama vile Syria, Iraq, Yemen, Tunisia, Libya Lebanon na
Misri hayana maslahi kwa mataifa hayo bali yanaongeza maafa kwa nchi na
wananchi na kuzinufaisha nchi za Magharibi na hasa Marekani na utawala
wa Kizayuni wa Israel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment