Turki al Feisal Mkuu wa zamani wa Shirika la Kijasusi la Saudi Arabia
ametaka makundi ya kigaidi nchini Syria yapewe silaha zaidi za kisasa
ili yakabiliane vilivyo na majeshi ya nchi hiyo. Al Feisal amekiri
kwamba waasi hawana uwezo wa kukabiliana na jeshi la Syria na kuongeza
kuwa makundi ya waasi yanayopambana na majeshi ya Syria lazima yapewe
silaha na zana za kisasa za kivita zikiwemo za kutungulia ndege na
vifaru. Turki al Feisal amepinga vikali kutumiwa njia za kidiplomasia za
kuutatua mgogoro wa Syria na kuongeza kuwa, kuna udhaura wa kupewa
waasi silaha za kisasa za kukabiliana na majeshi ya Syria.
Hivi
karibuni, Walid Muallim Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Syria
amesisitiza juu ya kukomeshwa usaidizi wa kifedha na kisilaha kwa
makundi ya kigaidi nchini humo kwa lengo la kutatuliwa mgogoro wa Syria
na kuongeza kuwa nchi za Qatar, Uturuki na Saudi Arabia zikiongozwa na
Marekani zimekuwa zikitoa uungaji mkono mkubwa wa kifedha na kisilaha
kwa makundi ya waasi na kigaidi nchini Syria.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment