Wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika watajadili migogoro na vita
vinavyoendelea kujiri nchini Mali, hitilafu baina ya Sudan na Sudan
Kusini, mapigano ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,
Guinea Bissau na Jamhuri ya Afrika ya Kati kwenye kikao kitakachoanza
kesho huko Addis Ababa mji mkuu wa Ethiopia. Tarifa zinasema kuwa,
mapigano ya Mali na mpango wa kutumwa kikosi cha Umoja wa Afrika kwa
shabaha ya kupambana na makundi yenye misimamo ya kufurutu mipaka
kaskazini mwa nchi hiyo, ni miongoni mwa ajenda kuu za kikao cha wakuu
wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika.
Hali kadhalika kikao hicho ambacho
kitahudhuriwa pia na Ban Ki moon Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,
kinatarajiwa kumpa uwenyekiti wa mzuguko wa Umoja wa Afrika Haile Mariam
Desalegne Waziri Mkuu wa Ethiopia kutoka kwa Rais Thomas Yayi Boni wa
Benin. Kikao cha wakuu wa wanachama wa Umoja wa Afrika kitaanza kesho
Jumapili na kuendelea hadi Jumatatu nchini Ethiopia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment