Watu wasiopungua 36 wamefariki dunia na wengine wapatao elfu sabini
wamekosa makaazi baada ya kunyesha mvua kubwa iliyosababisha kutokea
mafuriko nchini Msumbiji. Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Msumbiji
imeeleza kuwa, watu 26 wamepoteza maisha katika eneo la kusini mwa jimbo
la Gaza pekee. Mafuriko hayo yanatokana na mvua kubwa zilizonyesha
katika nchi za Afrika Kusini na Zimbabwe na kusababisha kufurika maji
katika Mto Limpopo. Nchi Afrika Kusini nako wiki iliyopita watu 12
walipoteza maisha baada ya kutokea mafuriko nchini humo. Brigedia
Jenerali Xolani Mabanga wa jeshi la Afrika Kusini amesema kuwa, nchi
hiyo imetuma helkopta mbili za kijeshi na kikosi cha waokoaji kwa lengo
la kuwasidia wananchi wa Msumbiji waliokumbwa na maafa hayo. Aidha
Afrika Kusini imetuma ndege ya kijeshi ikiwa na timu za madaktari,
wauguzi na wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu kwa lengo la kuwasaidia
wananchi wa Msumbiji.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment