Waziri wa Ulinzi wa Iran Brigedia Jenerali Ahmad Vahidi amesema
kuwa kuwepo majeshi ya kigeni katika eneo la Ghuba ya Uajemi kuna
madhara kwa mataifa ya eneo hili.
Meja Jenerali Vahidi ambaye alikuwa akizungumza katika kikao cha
mwisho cha mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya majeshi ya nchi
za Kiislamu mjini Tehran ametahadharidha juu ya hatari za kuwepo majeshi
ya kigeni katika eneo hili na ameziusia nchi za eneo hilo kufanya
jitihada za kuwafukuza wanajeshi wa nchi za kigeni katika maeneo yao.
Wakati huo huo Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu
(SEPAH) Brigedia Jenerali Hussein Salami amesema katika shehehe za
kufunga mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya majeshi ya nchi za
Kiislamu kwamba nchi za kibeberu zinafanya njama kubwa za kuzusha
hitilafu na mifarakano ya kidini na kimadhehebu katika nchi za Waislamu.
Salami amesema mashindano ya kimataifa ya Qur'ani kwa ajili ya majeshi
ya nchi za Waislamu ya Tehran ni nembo ya umoja na mshikamano ya
yamefanyika kwa lengo la kuzima njama hatari za maadui wa umma wa
Kiislamu.
No comments:
Post a Comment