Baada ya kurejea nchini kwake akitokea Afghanistan alikokwenda
kuhudumu kwa kipindi cha miezi mitano, mrithi nambari tatu wa utawala wa
Uingereza Prince Harry amesema kuwa aliua Waislamu ili kulinda watu wa
taifa lake. Harry amesema alikuwa akiua watu huko Afghanistan kwa ajili
eti ya kuokoa maisha ya watu wa Waingereza.
Hadi sasa haijabainika ni Waislamu wangapi wa Afghanistan waliouawa
na mwanamfalme huyo wa Uingereza akitumia helikopta ya kijeshi ya Apache
ambako amekutaja kuwa "kunamfurahisha" sawa kabisa na kuchezo mchezo wa
video. Amesisitiza kuwa alifurahia kuua watu kwa kutumia helikopta kwa
kuwa kitendo hicho kwake ni sawa na kucheza mchezo anaoupendelea wa
video kwa kutumia PlayStation au Xbox.
Maelfu ya raia wasiokuwa na hatia wa Afghanistan wameuawa katika
mashambulizi yanayoendelea kufanywa na majeshi ya nchi za Magharibi
dhidi ya maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment