Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergei Lavrov ameonya kuwa hujuma yoyote ya kijeshi dhidi ya Iran itasababisha maafa makubwa.
Akizungumza na waandishi habari mjini Moscow, Lavrov amesema kutatua
kadhia ya nyuklia ya Iran kupitia nguvu za kijeshi ni jambo ambalo
litasababisha maafa makubwa duniani.
Kwingineko katika matamshi yake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia
amesema Iran ina nafasi muhimu sana katika kutatua matatizo ya Mashariki
ya kati. Lavrov amesisitiza kuwa bila kuhusishwa Iran, matatizo mengi
ya eneo hilo hayawezi kutatuliwa.
No comments:
Post a Comment