Wabunge kadhaa nchini Uhispania wameikosoa vikali serikali ya nchi hiyo
kwa kupiga marufuku matangazo ya kanali za Televisheni za Press TV na
Hispan TV kutokana na mashinikizo ya lobi za Kizayuni na Marekani.
Katika barua yao, wabunge wa chama cha United Left wameitaka serikali ya
Uhispania kutoa maelezo iwapo Waziri wa Mambo ya Nje wa Uhispania Jose
Manuel Garcia-Margallo alijadili suala la kupiga marufuku kanali za Iran
wakati alipokutana na lobi za Kizayuni Oktoba mwaka 2012.
Wabunge hao
wamesema mmiliki wa shirika la satalaiti ya Eutelsat ana uraia wa Israel
na kwamba amekuwa akiongoza njama dhidi ya vyombo vya habari vya Iran
barani Ulaya. Televisheni ya Iran ya Hispan TV hurusha matangazo kwa
lugha ya Kihispania kwa masaa 24 nayo Press TV hurusha matangazo yake
kwa lugha ya Kiingereza. Hivi karibuni televisheni za kimataifa za Iran
Hispan TV pamoja na Press TV zilipigwa marufuku kurusha matangazo yao
kupitia satalaiti za Ulaya za Eutelsat na Hotbird. Aidha Shirika la
Intelsat limepiga marufuku matangazo ya radio na televisheni kadhaa za
kimataifa za Iran kufuatia mashinikizo ya Umoja wa Ulaya. Maamuzi hayo
ya kupiga marufu vyombo vya habari vya Iran ni ishara ya wazi ya
undumakuwili wa nchi za Magharibi zinazodai kutetea uhuru wa maoni. Nchi
za Ulaya na Marekani zikishirikiana na utawala wa Kizayuni wa Israel
zinajaribu kuzima sauti ya haki ya vyombo vya habari vya Iran.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment