Madaktari wa Bahrain wanakabiliwa na mateso makali wakiwa jela na
korokoroni kwa kosa la kuwatibu wapinzani wa serikali ya nchi hiyo.
Daktari Nada Dhwayf amesema kuwa, katika kipindi alichowekwa mahabusu
alikabiliwa na mateso makubwa kutoka vikosi vya usalama vya utawala wa
Aal Khalifa wa nchi hiyo kwa kosa la kuwapa matibabu wanamapambano wa
nchi hiyo. Daktari Dhwayf ameongeza kuwa, familia ya Aal Khalifa ndio
inayopaswa kubebeshwa lawama za ukatili unaofanywa dhidi ya madaktari na
wauguzi nchini humo.
Tokea kuanza kwa vuguvugu la mageuzi nchini Bahrain mwezi Februari
mwaka 2011, karibu madaktari elfu mbili wameshatiwa mbaroni na suala
hilo limesababisha wananchi wengi kupoteza maisha yao kwa kukosa huduma
za tiba.
No comments:
Post a Comment