Harakati ya Jihadul Islami ya Palestina imelaani vikali matamshi
yaliyotolewa na Rais Mahmoud Abbas wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina
kuhusiana na mpango wa kuundwa serikali mbili za Palestina.
Khadhwar Habib mmoja kati ya viongozi waandamizi wa Jihadul Islami ya
Palestina amesema kuwa, matamshi ya Mahmoud Abbas ya kutaka kuundwa
serikali mbili za Palestina yanakinzana na malengo ya muqawama na
mapambano ya wananchi wa Palestina dhidi ya Wazayuni, kwani mapambano
ndiyo njia pekee itakayoweza kuzikomboa ardhi za Palestina zinazokaliwa
kwa mabavu na utawala wa ghasibu wa Israel.
Habib amekosoa vikali msimamo wa Rais wa Mamlaka ya Ndani ya
Palestina na kuongeza kuwa, ardhi ya kihistoria ya Palestina
imeshikamana na kamwe wananchi wa Palestina hawako tayari kuutambua
rasmi utawala wa Kizayuni wa Israel.
No comments:
Post a Comment