Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayeshughulikia masuala ya
nchi za Kiarabu na Kiafrika amesema kuwa, Tehran ipo tayari kutuma
misaada ya kibinadamu kwa wakimbizi wa Syria walioko nchini Jordan
kupitia Jumuiya ya utoaji misaada ya Hilali Nyekundu. Hussein
Amir-Abdullahian amesema hayo alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa
Jordan Nasser Jouder mjini Amman. Aidha kuhusiana na mgogoro wa Syria
amesema kuwa, nchi za Magharibi na Marekani ndio wafadhili wakuu wa
makundi ya kigaidi nchini Syria kwa sababu zinayapa silaha zinazotumiwa
kuua watu na kuharibu miundombinu ya Syria.
Katika upande mwingine utawala wa Kizayuni wa Israel umepeleka
makombora katika eneo la Haifa karibu na mpaka wa Syria, hatua ambayo
imedaiwa na utawala huo kuwa ni jambo la kawaida. Hatua hiyo
imechukuliwa siku kadhaa baada ya Jumuiya ya Kijeshi ya Nato kuweka
mitambo ya makombora katika mpaka wa Uturuki na Syria, suala ambalo
Damascus imelipinga na kusema ni uchokozi.
No comments:
Post a Comment