Mbunge wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo anayetuhumiwa kushirikiana na waasi wa M23 amekimbilia Ufaransa baada ya kuwa nchini Burundi kwa mwezi mmoja. Roger Lumbala anatafutwa na serikali ya Kinshasa kwa tuhuma za kushirikiana na waasi wa M23 wanaopigana na serikali mashariki mwa nchi hiyo. Mwezi uliopita, Roger Lumbala alikimbilia kwenye ubalozi wa Afrika Kusini mjini Bujumbura, Burundi na kuomba hifadhi.
Habari zinasema kuwa mbunge huyo aliondoka katika ubalozi wa Afrika Kusini mjini Bujumbura siku ya Jumamosi na kuelekea uwanja wa ndege ambapo alisafiri hadi Ufaransa akitumia ndege ya Kenya Airways. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imesakamwa na machafuko tangu kutokea uasi jeshini mwanzoni mwa mwaka huu ambapo Jenerali Bosco Ntaganda aliondoka kambini na zaidi ya askari 200 na kuingia msituni baada ya kutokea mgongano kati yake na Rais Joseph Kabila.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment