Kushambuliwa kwa ubalozi wa Marekani mjini Cairo kumesababisha kuongezeka mashinikizo ya Warepublican kwa Rais wa Marekani Barack Obama ya kumtaka asimamishe msaada wa fedha wa serikali ya Washington kwa Misri. Kusambazwa kwa filamu inayoyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu, kumesababisha maelfu ya Waislamu nchini Misri kufanya maandamano makubwa mbele ya ubalozi wa Marekani nchi ambayo kulitengenezwa na kusambazwa filamu hiyo. Katika maandamano hayo ubalozi huo wa Marekani mjini Cairo ulishambuliwa na Wamisri wenye hasira. Shambulio hilo limekuwa uwanja mpya kwa ajili ya mpambano wa uchaguzi kati ya Warepublican na Wademocrats nchini Marekani.
Mitt Romney mpinzani wa Obama na mgombea urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican katika uchaguzi wa tarehe sita Novemba mwaka huu, ameshadidisha na kuelekeza mashambulizi yake kwa siasa za nje za utawala wa Obama, kwa kisingizio cha kuuawa wanadiplomasia wanne wa Marekani nchini Libya na kushambuliwa kwa balozi za nchi hiyo huko Yemen na Misri. Mitt Romney anadai kwamba, Rais Barack Obama wa Marekani hajachukua hatua kali kufuatia kuuawa kwa wanadiplomasia wa nchi hiyo huko Libya au kushambuliwa kwa balozi za Washington katika nchi mbalimbali duniani. Aidha mgombea huyo wa urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican ameitaka serikali ya Washington kusimamisha msaada wa fedha wa kila mwaka inaotoa kwa Misri. Amesema ikiwa Misri inataka iendele kupata msaada huo wa dola bilioni 1.3 lazima ikubaliane na masharti maalumu na ithibitishe kivitendo kuwa inayatekeleza masharti hayo ya Washington. Miongoni mwa masharti hayo ni kulinda usalama wa balozi za nchi mbalimbali zilizopo Misri ukiwemo ubalozi wa Marekani. Aidha kufungamana serikali mpya ya Cairo na mkataba wa Camp David wa makubaliano ya amani kati ya nchi hiyo na utawala haramu wa Israel. Na sharti jengine lililotajwa na Mitt Romney, ni kudhamini haki za jamii za dini zenye wafuasi wachache nchini humo. Bila shaka kwa muda wa miongo mitatu serikali ya Marekani ilikuwa ikiupatia misaada ya fedha utawala wa kidikteta wa Hosni Mubarak bila ya kuuwekea masharti yoyote. Kwa hakika sehemu kubwa ya misaada ya fedha iliyokuwa ikitolewa na Marekani ilikuwa ya silaha ambayo ilidhamini kuendelea kubaki madarakani utawala wa kidikteta wa Mubarak. Ukweli ni kwamba hivi sasa si Warepublican pekee lakini hata Wademocrat wanaotawala Marekani wana shaka na msimamo wa Misri mpya kuhusiana na Israel. Na hata katika mahojiano aliyofanyiwa hivi karibuni Obama amesema haihesabu tena Misri kuwa muitifaki wa Marekani japokuwa haichukulii pia kuwa ni adui wa Washington. Obama ameongeza kwamba radiamali ya serikali ya Cairo kuhusiana na matukio ya hivi karibuni, yaani kushambuliwa ubalozi wa Marekani mjini Cairo ndio itakayoainisha aina ya uhusiano wa serikali ya Misri na Washington baada ya utawala wa Mubarak. Kwa maneno mengine ni kuwa hivi sasa Rais wa Marekani anasubiri kuona msimamo wa rais mpya wa Misri Muhammad Mursi juu ya baadhi ya masuala kama vile uhusiano wa nchi hiyo na Israel na jinsi atakavyoamiliana na Wamisri wanaoipinga Marekani ili kuweza kujua kama je Misri ingali ni miongoni mwa marafiki wa karibu wa Washington katika Ulimwengu wa Kiarabu na wa Kiislamu, au imeamua kufuata njia nyengine? Kama serikali mpya ya Misri itaamua kufuata njia inayokinzana na matakwa na maslahi ya Marekani katika Mashariki ya Kati msimamo wa Washington ni kuitia adabu kwa kuikatia misaada ya fedha
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment