Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Monday, September 17, 2012

Rais aliyeshindwa Somalia alijaribu kunihonga

Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Prof. Sam Ongeri amefichua kwa mara ya kwanza juhudi zilizofanywa na Rais aliyeshindwa uchaguzini huko Somalia za kujaribu kubakia madarakani. Prof. Ongeri amesema kuwa, Sheikh Sharif Sheikh Ahmed alimpigia simu kabla ya uchaguzi na kuzungumza naye kwa zaidi ya saa moja ambapo alitaka Kenya itoe msimamo wa wazi wa kumuunga mkono. Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya ameongeza kuwa, Sheikh Ahmed alionyesha nia ya kutaka kumpa hongo ili afanikishe suala hilo.
Ongeri amekwenda mbali na kusema kuwa, kuna uwezekano kwamba rais huyo anayeondoka ana mkono katika jaribio la mauaji dhidi yake na Rais mpya wa Somalia kwani baada ya kukataa ombi la kumuunga mkono, Sheikh Sharif alikasirika na kukatiza mazungumzo. Huku hayo yakijiri, Rais mpya wa Somalia ameapishwa leo na kuchukua rasmi hatamu za uongozi mjini Mogadishu. Hassan Sheikh Mohamud ameahidi kushirikiana na Wasomali pamoja na jamii ya Kimataifa kuijenga upya nchi hiyo ya Pembe ya Afrika ambayo imeharibiwa na vita vya zaidi ya miongo miwili.

No comments: