Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Monday, September 17, 2012

IAEA iko tayari kuendelea kufanya mazungumzo na Iran

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki amesema IAEA una nia thabiti ya kuendelea kuzungumza na Iran ili kutatua kadhia ya nyuklia ya Tehran. Yukiya Amano amesema hayo leo katika mkutano wa mwaka wa wakala huo. Amano ameongeza kwamba wakala huo utafanya mazungumzo zaidi na Iran kwa lengo la kuondoa wasiwasi kuhusiana na shughuli za Tehran za nishati ya nyuklia. Duru ya mwisho ya mazungumzo kati ya Iran na wakala wa IAEA ilifanyika mwezi Agosti mjini Vienna, Austria na kabla ya hapo wawakilishi wa pande mbili walifanya duru mbili za mazungumzo mwezi Januari na Februari. Iran inasisitiza kwamba, kwa kuwa imesaini Makubaliano ya Kuzuia Uzalishaji na Usambazaji wa Silaha za Nyuklia NPT na ni mwanachama wa wakala wa IAEA hivyo ina haki ya kustafidi na teknolojia ya nyuklia kwa malengo ya amani.

No comments: