Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Sunday, September 23, 2012

Binti ajifungua mtoto wakati akifanya mtihani wa darasa la saba

Mwanafunzi ajifungua wakati akifanya mtihani wa darasa la saba. Tukio hilo limetokea katika Shule ya Msingi Kabiri, iliyopo katika wilaya ya Muleba mkoani Kagera. Mwanafunzi huyo, mwenye umri wa miaka 14 alijifungua wakati akifanya mtihani wa pili na wenzake ndani ya chumba cha mtihani.
Kwa mujibu wa habari zilizotoka shuleni hapo, muda mfupi baada ya kuanza mtihani wa Hisabati, mwanafunzi huyo alimwomba Msimamizi amruhusu kutoka nje kwa kuwa alikuwa akijisikia vibaya. Msimamizi alimnyima rukhsa akidhani ni ujanja wa ku-cheat mtihani lakini baadaye msimamizi alimuona mwanafunzi huyo akijinyonganyonga.

“Msimamizi alimwuliza anaumwa nini akamwambia anaumwa tumbo na baada ya kuendelea kumhoji alimweleza wazi kwamba anaumwa uchungu, hali iliyomfanya Msimamizi aende kwa mmoja wa walimu wa shule hiyo na kumwomba msaada,” alisema mmoja wa watahiniwa hao.
Aliongeza: “Walimchukua na kumwingiza kwenye nyumba ya mwalimu huyo na kumfuata mkunga wa jadi ambaye alimsaidia kujifungua salama mtoto wa kiume”.
Akizungumzia tukio hilo, Kaimu Ofisa Elimu wa Wilaya ya Muleba, Savera Celestine alithibitisha binti huyo kujifungua

1 comment:

AO Secretarial & Technology Supplies said...

inasikitisha sana kwa mtoto wa Darasa la Saba kufanya mtihani akiwa ni mjamzito......