Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Sunday, September 23, 2012

Walimu Kenya wakataa ofa na kubeza tishio la serikali

Walimu nchini Kenya wamekataa ofa ya serikali ya nchi hiyo ya kulipwa shilingi bilioni 13.5 ambazo zingetolewa kwa awamu tatu kuanzia mwezi ujao wa Oktoba. Chama cha Kitaifa cha Walimu nchini Kenya (KNUT) kimekataa kusitisha mgomo ambao umeendelea kwa wiki tatu sasa. Wakuu wa Chama cha Kitaifa cha Walimu nchini Kenya waliokutana Nairobi leo wamekataa katakata ofa ya Baraza la Mawaziri ya siku ya Alkhamisi na kusema kwamba, serikali haikuwachukulia kwa uzito kama inavyopaswa.
Wakati huo huo Chama cha Kitaifa cha Walimu nchini Kenya (KNUT) kimebeza tishio la serikali la kuwafuta kazi na kimemtaka Waziri wa Elimu Bw. Mutula Kilonzo atekeleze vitisho vyake vya kuwafuta kazi na kubainisha kwamba, walimu anaodhamiria kuwaajiri wataungana na walimu wengine katika mgomo. Serikali ya Kenya imeonya kuwa itawafuta kazi walimu wasiorejea katika vituo vyao vya kazi kufikia Jumatatu ya keshokutwa. Serikali ya Kenya imeonya kuwa itawafuta kazi walimu hao na kuajiri wengine wapya waliofuzu kutoka vyuoni na wale waliostaafu; hata hivyo walimu wanaoendelea na mgomo katika skuli za umma wamesisitiza kwamba, hawatishiki na hilo na kwamba, mgomo ungali unaendelea.

No comments: