Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC),
katika kujibu vitisho vya utawala haramu wa Israel dhidi ya Iran,
amesema kuwa Israel ikiihujumu Iran basi huo utakuwa mwanzo wa kuangamia
kwake.
Akizungumza mjini Tehran siku ya Jumamosi, Meja Jenerali Mohammad
Jafari amesema ‘vita dhidi ya Iran hatimaye vitajiri lakini bado
haijabainika vitakuwa lini na wapi.’
Amesisitiza kuwa Iran iko tayari
kukabiliana na tishio lolote dhidi yake. Kamanda huyo ameongeza kuongeza
kuwa Israel ambayo ni ‘donda la saratani’ imeamua kuwa njia pekee ya
kukabiliana na Iran ni kuanzisha vita. Aidha amewataja viongozi wa
Israel kuwa wajinga sana na kwamba mabwana zao wanapaswa kuwazuia.
Meja Jenerali Mohammad Jafari amesema Mapinduzi ya Kiislamu
yamechukua mkondo wa kasi katika kufikia malengo yake jambo ambalo
Wazayuni wameshindwa kulistahamili na kwa hivyo wanataka kuanzisha vita.
Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema Jeshi la
Iran lina uwezo kamili wa kukabiliana na adui. Utawala haramu wa Israel
umekuwa ukitoa vitisho vya kushambulia kijeshi vituo vya nyuklia vya
Iran kabla ya uchaguzi wa rais wa Marekani utakaofanyika Novemba 6.
Ikumbukwe kuwa mpango wa nyuklia wa Iran wenye malengo ya amani
unafanyika kwa mujibu wa sheria za kimataifa.
No comments:
Post a Comment