Mwanafunzi ajifungua wakati akifanya mtihani wa darasa la saba. Tukio
hilo limetokea katika Shule ya Msingi Kabiri, iliyopo katika wilaya ya
Muleba mkoani Kagera. Mwanafunzi huyo, mwenye umri wa miaka 14
alijifungua wakati akifanya mtihani wa pili na wenzake ndani ya chumba
cha mtihani.
Kwa mujibu wa habari zilizotoka shuleni hapo, muda mfupi baada ya
kuanza mtihani wa Hisabati, mwanafunzi huyo alimwomba Msimamizi amruhusu
kutoka nje kwa kuwa alikuwa akijisikia vibaya. Msimamizi alimnyima
rukhsa akidhani ni ujanja wa ku-cheat mtihani lakini baadaye msimamizi
alimuona mwanafunzi huyo akijinyonganyonga.
“Msimamizi alimwuliza anaumwa nini akamwambia anaumwa tumbo na baada
ya kuendelea kumhoji alimweleza wazi kwamba anaumwa uchungu, hali
iliyomfanya Msimamizi aende kwa mmoja wa walimu wa shule hiyo na
kumwomba msaada,” alisema mmoja wa watahiniwa hao.
Aliongeza: “Walimchukua na kumwingiza kwenye nyumba ya mwalimu huyo
na kumfuata mkunga wa jadi ambaye alimsaidia kujifungua salama mtoto wa
kiume”.
Akizungumzia tukio hilo, Kaimu Ofisa Elimu wa Wilaya ya Muleba, Savera Celestine alithibitisha binti huyo kujifungua
1 comment:
inasikitisha sana kwa mtoto wa Darasa la Saba kufanya mtihani akiwa ni mjamzito......
Post a Comment