Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Sunday, July 22, 2012

Marekani imeanzisha kampeni ya kuitenganisha Iran na Kenya

Balozi wa Iran nchini Kenya amelaani vikali njama za kimataifa za Marekani za kutaka Kenya na nchi zingine duniani zijitenge na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Katika mahojiano maalumu na gazeti la Standard on Sunday la mjini Nairobi, Balozi wa Iran nchini Kenya Malek Hossein Givzad ameongeza kuwa Marekani inashirikiana na utawala haramu wa Israel na baadhi ya nchi za Umoja wa Ulaya katika kueneza madai yasiyo na msingi kuwa eti Iran inaunga mkono ugaidi. Amesema madai hayo yanakusudia kuiharibia jina Iran katika uga wa kimataifa.

Mapema mwezi huu Kenya ilibatilisha mkataba iliotia saini na Iran kuhusu kununua mamilioni ya tani za mafuta ghafi ya Iran. Givzad amesema Kenya ilibatilisha mkataba huo kutokana na mashinikizo ya Marekani. Ameongeza kuwa yamkini Kenya ikajuta kupoteza fursa hiyo nzuri ya kununua mafuta ya Iran. Hata hivyo Balozi Givzad amesema mashinikizo hayawezi kuvuruga uhusiano mzuri wa Iran na Kenya. Ameongeza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendelea kuwekeza nchini Kenya katika sekta za biashara, utalii, huduma za uhandisi, elimu, kilimo na viwanda. Kuhusu kesi ya Wairani wawili waliokamatwa mwezi uliopita nchini Kenya, Balozi Givzad amesema hiyo ni njama iliyopangwa na nchi za Magharibi kwa lengo kuharibu jina la Iran.

No comments: