
Rais amesema hayo katika ufunguzi wa Maonyesho ya 20 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yaliyoanza jana hapa mjini Tehran.
Ufunguzi wa maonyesho hayo umekwenda sambamba na sherehe za 18 za kuwakirimu watu wanaotumikia Qur'ani Tukufu, sherehe ambazo zimehudhuriwa pia na wasomi, wanaharakati wa kada na fani mbalimbali za Qur'ani, watumishi wa Qur'ani Tukufu, mahafidhi wa ndani na nje ya Iran na wakuu wa taasisi mbalimbali za Qur'ani nchini Iran.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pia amesema, ni jambo muhimu na la busara sana kufanyika maonyesho kama hayo na kusisitiza kuwa, kurejea kwenye utamaduni wa Qur'ani, kujipamba kwa sifa za mwanadamu kamili na kushikamana na njia ya Mtume Muhammad SAW ndio utatuzi pekee wa matatizo yote yanayoukabili ulimwengu hivi sasa.
No comments:
Post a Comment