skip to main |
skip to sidebar
Waasi wa Kongo wadhibiti eneo moja karibu na mpaka wa Rwanda
Umoja wa Mataifa na maafisa wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wameripoti kuwa, waasi wa mashariki mwa nchi hiyo wamedhibiti eneo moja karibu na mpaka wa Rwanda baada ya kuvishambulia vikosi vya serikali. Alex Essome, msemaji wa mpango wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda amani Kongo katika eneo la Goma amesema, waasi wa M23 wamedhibiti vijiji vitano na kwamba jeshi linafanya jitihada la kukomboa vijiji hivyo kutoka mikononi mwa waasi. Ameongeza kuwa, waasi hao wamevisababishia vikosi vya jeshi la Kongo hasara kubwa na kupora kiasi kikubwa cha silaha wakati wa mapigano hayo yaliyojiri juzi Alkhamisi. Jimbo la Kivu Kaskazini limekuwa likikabiliwa na wimbi la machafuko tangu mwezi Machi, baada ya maelfu ya askari kuasi jeshini na kujiunga na Jenerali muasi Bosco Ntaganda. Inadaiwa kuwa Jenerali Bosco Ntaganda ni Mnyarwanda na serikali ya Rwanda pia inatuhumiwa kuwasaidia waasi hao. Hata hivyo Kigali imekanusha kuwasaidia waasi wa Congo.
No comments:
Post a Comment