Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Thursday, June 14, 2012

‘Russia inapinga vikwazo dhidi ya Iran’


Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergei Lavrov amesema Moscow inapinga vikwazo vya upande moja dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Akizungumza na waandishi habari baada ya kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Ali Akbar Salehi, Lavrov ameelezea matumaini kuwa mazungumzo yajayo ya Iran na kundi la 5+1 mjini Moscow yatazaa matunda na kuondoa suutafahamu zilizopo. Lavrov aliwasili Tehran siku ya Jumatano kwa lengo la kufanya mazungumzo na wakuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Kuhusiana na kadhia ya Syria, Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni nchi yenye ushawishi katika eneo na ina nafasi muhimu katika kutatua mgogoro wa Syria. Amesema Russia itaandaa kongamano la kimataifa kuhusu Syria ambapo Iran itashirikishwa. Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia pia ameituhumu Marekani kuwa inawapatia silaha waasi nchini Syria.
Lavrov amesema Russia ina msimamo sawa na Jamhuri ya Kiisalmu ya Iran kuhusu Syria. Amesema kuwa Moscow inaunga mkono mpango wa amani wa Kofi Annan nchini Syria.
 

No comments: