
Ali Akbar Velayati , mshauri wa ngazi za juu wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa Israel au nchi nyingine yeyote haina uwezo wa kuishambulia kijeshi Iran kwani Iran ni nchi yenye nguvu na uwezo mkubwa katika eneo. Velayati ambaye aliwahi kuwa waziri wa mambo ya nje wa Iran ameyasema hayo katika mahojiano na gazeti la Al Jamhuriyah la Lebanon.
Amesema iwapo yeyote atathubutu kufanya kitendo cha wendawazimu cha kuishambulia Iran kijeshi, atapata somo ambalo hatalisahau. Wakuu wa Marekani na utawala haramu wa Israel mara kwa mara wamekuwa wakitoa vitisho vya kuishambulia Iran kijeshi ili kuilazimisha Jamhuri ya Kiislamu isitishe mpango wake wa nyuklia wenye malengo ya amani. Wazayuni na Wamarekani wanadai kuwa mpango wa nyuklia wa Iran una malengo ya kijeshi. Iran imekanusha madai hayo na kusisitiza kuwa shughuli zake za nyuklia zinafanyika chini ya uangalizi wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA ambao umetoa ripoti kadhaa na kuthibitisha kuwa shughuli za nyuklia za Iran hazijakiuka mkondo wa amani.
No comments:
Post a Comment