Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Thursday, June 14, 2012

Ben Ali wa Tunisia ahukumiwa kifungo cha miaka 20 jela kwa kuchochea mauaji

Mahakama moja ya kijeshi nchini Tunisia imemhukumu dikteta wa zamani wa nchi hiyo Zine El Abidine Ben Ali miaka 20 jela kwa kuchochea mauaji na vitendo vingine kadhaa vya uhalifu.
Katika hukumu hiyo iliyotolewa Jumatano, Ben Ali amepatikana na hatia ya ‘kuchochea vurugu, mauaji na uporaji' katika mji wa Ouardanine mashariki mwa nchi hiyo.Ben Ali amehukumiwa bila kuwepo mahakamani kwani alikimbilia Saudi Arabia kufuatia mapinduzi ya wananchi wa Tunisia Januari 14, 2011.
Mwendesha mashtaka katika jeshi la Tunisia anasema Ben Ali anapaswa kuhukumiwa kifo kutokana na vifo alivyosababisha kote Tunisia katika mwamko wa wananchi mwaka jana.
Utawala wa Kifalme wa Saudi Arabia umekataa kumkabidhi Ben Ali kwa wakuu wa Tunisia licha ya kuwepo waranti wa kimataifa wa kutaka dikteta huyo wa zamani atiwe nguvuni.

No comments: