
Saeed Jalili amesema hayo katika wakati huu wa kukaribia mazungumzo kati ya Iran na kundi la 5+1 mjini Moscow Russia na kuongeza kuwa, Tehran inataraji kwamba, haki yake ya kufaidika na teknolojia ya nyuklia ukiwemo urutubishaji urani itatambuliwa rasmi na kuheshimiwa, hasa kwa vile suala hilo limeelezwa wazi katika Mkataba wa Kuzuia Uzalishaji na Uenezaji wa Silaha za Nyuklia N.P.T. Aidha amesisitiza kwamba Iran inapinga umilikaji wa silaha za mauaji ya umati zikiwemo za nyuklia na kwamba ina uwezo wa kushiriki harakati za kupokonya silaha hizo, hivyo, uwezo huo unapaswa kutumiwa na jamii ya kimataifa na kwamba kutambuliwa haki yake ya kurutubisha urani kutasaidia kupelekea mbele mazungumo hayo.
Mazungumo kati ya Iran na kundi la 5+1 yanayojumuisha nukta mbalimbali yatafanyika tarehe 18 na 19 mwezi huu wa Juni katika mji mkuu wa Russia, Moscow.
No comments:
Post a Comment