Ikulu ya Marekani, White House
Ikulu ya Marekani kwa mara ya kwanza imekiri kufanya mashambulizi na mauaji dhidi ya makundi inayodai kwamba ni ya wafuasi wa al Qaida nchini Yemen na Somalia. Katika ripoti yake ya nusu mwaka kwa bunge iliyotolewa jana Ijumaa, Ikulu ya Marekani imeeleza kile ambacho kimekuwa kikiripotiwa kwa miaka kadhaa lakini bila kukubaliwa na watawala wa Marekani kwamba, jeshi la nchi hiyo limekuwa likiwashambulia moja kwa moja wafuasi wa al Qaida nchini Yemen na Somalia.
Hata hivyo ripoti hiyo haikutaja ndege zisizo na rubani ambazo zimekuwa zikitumiwa na jeshi la Marekani kulenga maeneo mbalimbali ya Yemen na Mashambulizi hayo ya Marekani hasa yanayofanywa na ndege zake zisizo na rubani yamekuwa yakisababisha maafa na vifo vya idadi kubwa ya raia wasio na hatia katika nchi za Waislamu za Somalia, Yemen na Pakistan.

No comments:
Post a Comment