Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Tuesday, May 29, 2012

Shafiq ataka aya za Qur'ani ziondolewe katika vitabu vya shule Misri


Shafiq
Ahmad Shafiq, Waziri Mkuu wa mwisho wa utawala wa dikteta Hosni Mubarak nchini Misri. Ameahidi akishinda ataondoa aya za Qur'ani katika vitabu vya kufundishia mashuleni Misri.
Ahmad Shafiq aliyeingia katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais nchini Misri ametoa pendekezo la kushangaza la kutaka aya za Qur'ani Tukufu ziondolewe katika vitabu vya shule.
Imearifiwa kuwa katika mahojiano na televisheini ya Kikristo ya CTV, Shafiq aliyekuwa waziri mkuu wa mwisho wa dikteta Mubarak amedai kuwa sababu ya kuondolewa aya hizo ni kuwa ni vigumu kwa Wakristo kuzihifadhi!
Sheikh Yusuf Al Badri mmoja kati ya wahubiri wa Kiislamu Misri amesema matamshi ya Shafiq hayafai hasa kwa kuzingatia anagombea kiti cha urais. Duru ya pili ya uchaguzi wa rais Misri itafanyika Juni 16 na 17 ambapo Shafiq atachuana na mgombea wa Ikanul Muslimin Mohammad Morsi.
Maelfu ya watu wamefanya maandamano dhidi ya shafiq waziri mkuu wa mwisho wa utawala wa dikteta Hosni Mubarak mjini Cairo Misri na kuchoma moto ofisi yake ya kampeni.
Maafisa wa zimamoto walitumwa haraka kwenye ofisi hiyo na kufanikiwa kuzima moto huo.

No comments: