
Maafisa wa zimamoto walitumwa haraka kwenye ofisi hiyo na kufanikiwa kuzima moto huo.
Wakati huo huo jana Jumatatu miji yote ya Misri ilishuhudia maandamano ya wananchi ya kupinga matokeo yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi ya Misri.
Waandamanaji hao wanaamini kuwa tume hiyo imechakachua matokeo ya uchaguzi wa rais wa tarehe 23 na 24 mwezi huu wa Mei.
Mapema jana Faruq Sultan, mkuu wa tume ya uchaguzi ya Misri alitangaza matokeo rasmi ya uchaguzi huo ambapo mgombea wa Ikhwanul Muslimin Mohamed Morsi ameongoza akifuatiwa na Waziri Mkuu wa mwisho wa utawala wa dikteta Hosni Mubarak, Ahmad Shafiq.
Kwa mujibu wa matokeo hayo, hakuna mgombea aliyepata zaidi ya nusu ya kura zilizopigwa, hivyo wagombea hao wawili wameingia katika duru ya pili ya uchaguzi huo iliyopangwa kufanyika tarehe 16 na 17 mwezi ujao wa Juni.
No comments:
Post a Comment