Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Tuesday, May 29, 2012

BBC yalaumiwa kwa kueneza picha bandia za kuipaka matope serikali ya Syria


Televisheni ya utawala wa kifalme wa Uingereza BBC imelaumiwa kwa kutumia picha bandia iliyopigwa miaka 9 iliyopita nchini Iraq kwa ajili ya kuendeleza propaganda zake dhidi ya serikali ya Syria.
Gazeti la Daily Telegraph limeripoti kuwa, BBC imetumia picha ya zamani iliyopigwa mwaka 2003 nchini Iraq na kudai kuwa ni picha za watu waliouliwa na vikosi vya serikali nchini Syria.
Mpiga picha Marco Di Lauro aliyepiga picha hiyo huko Iraq mwaka 2003 amelalamika kwenye ukurasa wake wa Facebook akisema kama ninavyomnukuu: "Kuna mtu anatumia picha zangu kuendesha propaganda dhidi ya serikali ya Syria na kujaribu kuonesha serikali hiyo inafanya mauaji ya umati."
Wakati huo huo Bashar Ja'afari, Balozi wa Kudumu wa Syria katika Umoja wa Mataifa jana alilalamikia kile alichokiita ni "tsunami ya uongo" unaoenezwa na baadhi ya nchi na vyombo vya habari vya kieneo na kimataifa dhidi ya Syria.
Mapigano kati ya vikosi vya ulinzi vya Syria na makundi yenye silaha yamezuka tena licha ya kusimamishwa tarehe 12 Aprili mwaka huu chini ya mpango wa amani wa Kofi Annan, mpatanishi wa Umoja wa Mataifa katika mgogoro wa Syria.

No comments: