Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Friday, May 11, 2012

Velayati: Uistikabri wa kimataifa hautaki kuona ulimwengu wa Kiislamu ukiwa na nguvu

Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya kimataifa amesema kuwa, madola tajiri na yenye nguvu ulimwenguni hayataki kuona ulimwengu wa Kiislamu ukiwa na nguvu. Dakta Ali Akbar Velayati ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Mwamko wa Kiislamu amebainisha kwamba, mabeberu hawataki kabisa kuona nchi za ulimwengu wa Kiislamu zikiwa na ustawi na daima zinataka kuziona zikiwa dhaifu na tegemezi.
Ameongeza kwamba, hofu ya madola hayo ndio inayoyafanya yafanye kila njama ili kuzuia maendeleo na ustawi hasa wa kielimu wa nchi za Kiislamu. Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya kimataifa amebainisha kwamba, njia pekee ya kuyazuia madola ya kibeberu yasifikie malengo yao katika ulimwengu wa Kiislamu ni kujiimarisha kielimu na kiuchumi.

No comments: