Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametahadharisha kuhusiana na matokeo mabaya ya siasa za madola yenye kutaka kujitanua pamoja na ufisadi unaotawala ulimwenguni.
Rais Ahmadineja amesema hayo leo katika hadhara kubwa ya wananchi wa kaskazini mashariki mwa Iran na kuyatahadharisha madola hayo kwamba, muda si mrefu yatakumbwa na takdiri ya Mwenyezi Mungu pamoja na nguvu ya wananchi. Rais Ahmadinejad amesema, madola ya kibeberu ndio chanzo cha matatizo ya jamii ya mwanaadamu. Amesema, madola hayo yamesahau na kuacha njia ya Mwenyezi Mungu na kufuata njia ya shetani. Aidha Dakta Ahmadinejad amebainisha kwamba, daima fikra na vitendo vya madola yanayotaka kujitanua ni ufisadi, dhulma, mauaji, ubaguzi na udhalilishaji.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment