Serikali ya Tanzania imetangaza kuwapatia uraia wakimbizi wa Burundi wapatao 54,000 ambao wako katika kambi ya Bulyahulu Mkoani Tabora. Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhdumia Wakimbizi UNHCR, Wakimbizi hao waliingia Tanzania katika muongo wa 70 wakikimbia machafuko yaliyozuka nchini mwao.
Aidha serikali ya Tanzania imewapa uraia wakimbizi wengine kadhaa walio katika kambi za Katumba na Kishamo mkoani Rukwa Kaskazini mwa nchi hiyo. Hii ni mara ya pili wakimbizi wa waliokuwa kwenye makambi ya Tanzania wanapatiwa uraia baada ya kuishi nchini humo miaka mingi.
Wakizungumza na ujumbe wa UNHCR, wakimbizi kutoka Burundi wamesema wanajivunia kupata uraia wa Tanzania.

No comments:
Post a Comment