Rais wa Marekani Barack Obama amekataa kuidhinisha muswada wenye lengo la kuwasaidia wananchi wa bara la Afrika wanaokabiliwa na baa la njaa katika kikao cha viongozi wa G8. Hii ni katika hali ambayo, kabla ya kufanyika kikao hicho Barack Obama aliwasilisha muswada kwa ajili ya kukabiliana na umasikini barani Afrika sambamba na kuwasaidia watu wa bara hilo wanaokabiliwa na uhaba wa chakula na umasikini mkubwa. Obama alitangaza kuwa kwa uchache zilikuwa zinahitajika dola bilioni tatu kwa ajili ya kudhamini misaada kwa nchi masikini za Afrika sambamba na kuwataka viongozi wengine wa G8 kuchukua hatua kama hizo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment