
Ndege hizo za kigaidi za Marekani zilizopigwa marufuku, zimeshambulia mkoa wa Bayda wa kusini mwa Yemen na kuua Waislamu saba jana Jumatatu.
Marekani inadai shambulizi hilo lilimlenga kiongozi wa mtandao wa al Qaida katika mkoa wa Bayda, Qaed ad Dahab na ndugu yake wa kiume, lakini wote hao wawili wamekwepa shambulio hilo bila ya hata kujeruhiwa.
Jana Jumatatu pia, mashambulio mengine mawili ya ndege zisizo na rubani za Marekani yaliua Waislamu wasiopungua 12 karibu na mji wa Miranshah, kaskazini mwa Pakistan.
Nchini Afghanistan pia helikopta za kijeshi za Marekani zimefanya shambulio lililoua familia nzima ya raia wanane.
Msemaji huyo ameongaza kuwa, Shafi hakuwa mwanamgambo wa Taliban. Hakuwa mwanachama wa kundi lolote lile la wapinzani wa serikali, alikuwa mwanakijiji wa kawaida tu.
Kwa muda mrefu sasa Marekani imekuwa ikifanya mashambulizi katika nchi za Kiislamu za Pakistan, Afghanistan, Yemen na Somalia kwa madai ya kukabiliana na wanamgambo wa al Qaida. Hata hivyo Waislamu wa kawaida ndio wahanga wakuu wa mashambulio hayo ya Marekani.
No comments:
Post a Comment